Tusaidie kuboresha zana za Google for Education kwa ajili yako, wanafunzi na shule yako.
Tunathamini maoni yako
Iwe unatumia au hutumii bidhaa za Google, tungependa kupata maoni yako. Jisajili ili ushiriki katika utafiti wetu kuhusu watumiaji na uathiri jinsi timu zetu zinavyoboresha bidhaa ambazo mamilioni ya watu hutumia kila siku. Iwapo wasifu wako unafaa kwenye mojawapo ya tafiti zetu zijazo kuhusu watumiaji, utakuwa wa kwanza kujaribu ofa au vipengele vipya kwenye bidhaa kama vile Google Darasani, Chromebook na zaidi.
Kila mtu anayeshiriki katika utafiti wa kujitolea atapata kadi ya zawadi au mchango kwenye shirika alipendalo la misaada kama njia yetu ya shukrani.
Inafanyaje kazi?
Jisajili
Tupe maelezo machache kukuhusu kwa kujaza dodoso ili utusaidie kubainisha iwapo utafiti ujao utakufaa.
Shiriki
Iwapo wasifu wako unafaa, tutakutumia dodoso ya ufuatiliaji na maelezo kuhusu hatua zinazofuata, ikiwa ni pamoja na wakati na mbinu ya utafiti.
Pata zawadi
Furahia kadi ya zawadi au mchango kwenye shirika ulipendalo la misaada kama njia yetu ya shukrani. Tutakueleza mapema zawadi utakayopata.
Find out more
Kujisajili
Mnatafuta washiriki wa aina gani?
Wa aina zote. Si lazima uwe mtumiaji wa Google, mtaalamu wa kompyuta au mjuzi wa teknolojia ili ujisajili. Mtu yeyote aliye na umri wa zaidi ya miaka 18 na amewahi kutumia intaneti kwa njia yoyote anaweza kujiunga kwenye mpango huu.
Mtawasiliana nami baada ya muda gani?
Tunataka kuhakikisha kuwa utafiti unaofanya unakufaa. Ndiyo maana hatutoi hakikisho kuwa kila mtu atakayetuma ombi atashiriki kwenye utafiti. Iwapo tutawasiliana nawe, huenda hutaanza kushiriki mara moja kwa sababu tutakuwa tukisubiri utafiti utakaokufaa. Tunaweza kuwasiliana nawe wakati wowote mradi umejisajili.
Iwapo nitajisajili, mtanitumia barua taka au kuuza maelezo yangu kwa kampuni zingine?
Hapana. Maelezo yote unayotoa yanahifadhiwa kwa siri kulingana na Sera ya Faragha ya Google. Tutayatumia tu ili kutusaidia kupata washiriki wanaofaa kufanya utafiti wetu. Sisi au shirika la nje linalofanya kazi kwa niaba yetu, tutawasiliana nawe tu iwapo tunahitaji kukualika ushiriki katika utafiti au ikiwa utahitajika kufafanua baadhi ya maelezo uliyotoa.
Kwa nini Google inakusanya taarifa zangu binafsi kama vile kabila, jinsia, na hali ya ulemavu?
Google inakusudia kubuni hali za utumiaji wa bidhaa zinazojumuisha kila mtu. Ili kutekeleza suala hili ipasavyo, ni muhimu tupate maoni kutoka kwa kila mtu. Tunakusanya maelezo haya ili kuhakikisha kuwa tunapata kundi la washiriki linalowakilisha jamii nzima. Si lazima ujibu maswali yote na maelezo yako yanahifadhiwa kwa siri kulingana na Sera ya Faragha ya Google.
Nilijisajili, lakini nimeamua kuwa sihitaji kushiriki. Ninawezaje kujiondoa?
Unaweza kujiondoa wakati wowote kwa kujaza fomu ya kujiondoa.
Kushiriki katika utafiti
Nitakuwa nikifanya nini katika tafiti hizi?
Google inatekeleza aina mbalimbali za utafiti. Unaweza kualikwa ushiriki katika aina zozote za utafiti kati ya zifuatazo:
Utafiti kuhusu urahisi wa kutumia unaofanywa kutoka mbali
Katika tafiti hizi tutakusanya maoni yako kupitia kipindi cha kushiriki skrini pamoja na mtafiti ambapo unaweza kuulizwa maswali au kutoa maoni kuhusu kubuni au mchakato. Unaweza kushiriki utafiti huu kutokea karibia sehemu yoyote duniani, lakini utahitaji kuwa na muunganisho wa Intaneti wenye kasi ya juu.
Kutoa maoni katika ofisi ya Google
Hii inafaa zaidi kwa watu wanaoishi karibu na mojawapo ya ofisi zetu. Kwa kawaida, utakutana ana kwa ana na Mtafiti wa Google atakayekuuliza maswali kuhusu uzoefu wako katika kutumia bidhaa zetu au teknolojia kwa ujumla.
Ili kumlinda kila mtu katika kipindi cha janga la COVID-19, tafadhali angalia mwaliko katika huduma ya Anwani kwenye Google ili upate maelezo husika ya kuingia katika ofisi ya Google. Unaweza kujibu moja kwa moja kwenye mwaliko wako ikiwa una maswali yoyote.
Utafiti kupitia fomu ndefu
Utafiti huu unahitaji ufanye shughuli chache kila siku kwa siku au wiki kadhaa. Watafiti wa Google watakuuliza ili ujibu maswali au uandike madokezo kulingana uzoefu wako wa kutumia bidhaa.
Tafiti
Katika tafiti hizi tutakutumia tu fomu ya utafiti ili uijaze. Tafadhali kumbuka kuwa kwa kawaida hatutoi zawadi kwa kushiriki katika utafiti.
Zawadi ya shukrani
"Zawadi ya Shukrani" humaanisha nini?
Ni njia ya Google ya utoaji zawadi inayotumika kama njia ya kutoa shukrani kwa watu wanaoshiriki katika tafiti ili kusaidia kuboresha hali za utumiaji na bidhaa zetu.
Nitapokea zawadi yangu lini?
Iwapo kipindi chako kinastahiki kupewa zawadi ya shukrani, unapaswa kuipokea ndani ya siku tatu hadi tano za kazi baada ya kuikamilisha. Tafadhali kumbuka kwamba si washiriki wote watakaoshiriki katika utafiti watapokea zawadi ya shukrani.