Tungependa kupata maoni yako, ili tuendelee kubuni bidhaa za Google zinazokufaa. Utapata nafasi ya kuchangia kwenye vitu ambavyo mamilioni ya watu hutumia kila siku, kuanzia barua pepe na programu za kuongeza tija hadi zana za wasanidi programu na waelimishaji.
Hata kama hutumii bidhaa za Google kwa sasa, bado unaweza kujisajili ili upate fursa ya kushiriki katika utafiti wetu. Iwapo mojawapo ya tafiti zetu unakufaa, tutawasiliana nawe kwa kukupa maelezo na hatua zitakazofuata. Washiriki wengi watapokea zawadi ndogo ya shukrani.